BOOST SOKONI MEDIA
MAELEKEZO KWA DALALI/WAKALA
1. Ni nini?
Ni mtandao unaonadi bidhaa au mali mbalimbali kama vile nyumba,gari,vyumba vya kupanga na pikipiki.ofisi za boost sokoni zipo mwanza mabatini.
2. Wanafanyaje kazi?
Boost sokoni humuunganisha dalali katika mtandao ili aweke bidhaa alizonazo kwa njia ya picha na video hivyo kupitia mtandao mteja atawasiliana na boost sokoni ambao watamuunganisha na dalali anayehusika na bidhaa anayohitaji kwa kifupi boost sokoni utafuta na kuwaletea madalali wateja.
3. Dalali ufaidikaje?
· Boost sokoni watatatangaza bidhaa zake kwa namna zote hivyo kupata wateja haraka.
· Mteja atampa hela ya ukaguzi dalali(hela ya mguu)
· Dalali atapewa asilimia yake baada ya mauzo kulingana na makubaliano ya mali husika.
· Dalali hatalipia chochote kwa kuweka bidhaa zake mtandao wa boost sokoni.
4. Mauzo hufanyikaje?
· Mkataba wa mauziano utafanyikia katika ofisi za mwanasheria anayetambulika na serikali.
· Uhakiki wa nyaraka za mali utafanyika kabla ya mauziano.
· Utaratibu wa mauziano utaandaliwa na ofisi ya boost sokoni.
· Boost sokoni ni waaminifu na uheshimu sheria.
Kwa mawasiliano zaidi
0745 251274